Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Seneta Raja Nasir Abbas Jafari, Mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Waislamu Pakistan, katika hotuba yake sambamba na kuukubali mkataba wa kusitisha mapigano kati ya Pakistan na Afghanistan, ameutaja kuwa ni hatua ya msingi katika njia ya amani ya kudumu na uthabiti wa eneo, na kusisitiza kuwa mazungumzo na diplomasia ndizo njia zenye ufanisi zaidi za kutatua tofauti kati ya nchi, na ameonesha matumaini yake kuwa makubaliano haya yatakuwa mwanzo wa zama mpya za usalama, mshikamano na maendeleo ya pamoja kwa mataifa ndugu.
Seneta Raja Nasir Jafari, huku akionesha furaha yake kutokana na mafanikio ya upatanishi wa nchi ndugu za Qatar na Uturuki, alisema: “Kwa dhati kabisa naukubali mkataba wa kusitisha mapigano kati ya Pakistan na Afghanistan; mafanikio haya ni matokeo ya jitihada za kweli na diplomasia yenye ufanisi ya marafiki wetu wa eneo.”
Akaongeza: “Kutia saini kwa makubaliano haya ni ushahidi wa wazi wa umuhimu wa mazungumzo na diplomasia katika kutatua tofauti baina ya mataifa, na inaweza kuchukuliwa kuwa ni hatua ya kimsingi katika njia ya kufikia amani ya kudumu na uthabiti wa eneo.”
Katika sehemu ya mwisho ya hotuba yake, Seneta Raja Nasir Abbas Jafari alieleza matumaini yake kwamba serikali ya Afghanistan itashikamana na ahadi zake zote ili kuweka mazingira ya uthabiti, utulivu na ustawi wa pamoja baina ya mataifa mawili ndugu, na vilevile kwamba makubaliano haya yanaweza kuwa mwanzo wa zama mpya za usalama, mshikamano na maendeleo ya pamoja katika uhusiano wa mataifa mawili ya Kiislamu.
Maoni yako